Tuesday, November 03, 2015
HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega anawatangazia wananchi wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega, kutuma maombi ya nafasi ya kazi kama ifuatavyo:-


Dereva Daraja la II (Nafasi 3)

TGOS. A

SIFA ZA MUOMBAJI:

      i.        Awe na Elimu ya kidato cha nne (Form IV)

     ii.        Awe na leseni ya Daraja ‘c’

    iii.        Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali.

   iv.        Awe na cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II (Trade Test GradeII)

    v.        Awe na umri usiopungua miaka 45

MAJUKUMU YA KAZI:

      i.        Kuendesha magari madogo na makubwa (Malori)

     ii.        Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote

    iii.        Kufanya uchaguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo

   iv.        Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari

    v.        Kutunza na kuandika daftari la safari (Log – Book) kwa safari zote.

MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara wa serikali yaani TGOS A kwa Mwezi.

Application Instructions:

 Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, taaluma na Cheti cha kuzaliwa.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/11/2015 saa 9:30 alasiri.

Maombi yatumwe kwa kutumia Anwani ifuatayo :-


Mkurugenzi Mtendaji (W),

Halmashauri ya Wilaya ya Nzega,

S.L.P 4,

Nzega


Limetolewa na :

ABRAHAMAN H. MNDEME

MKURUGENZI MTENDAJI


NZEGA