Saturday, November 07, 2015
1
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo anakaribisha maombi ya watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi mbili (2):

1.    DEREVA – NAFASI MOJA (1)

MAJUKUMU YA KAZI
•    Kuendesha magari atakayo pangiwa na mwajiri wake.
•    Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya ukaguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unao hitaji matengenezo.
•    Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
•    Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.

SIFA ZA MWOMBAJI
•    Kuajiriwa wahitimu kidato cha nne IV.
•    Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali.
•    Wenye cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la II.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya serikali ngazi ya mshahara TGOS A.

2.    KATIBU MAHUSUSI DARAJA LA III – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
•    Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
•    Kutunza taarefa/kumbukumbu za matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
•    Kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
SIFA ZA MUOMBAJI

•    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo ya Uhazili kutoka chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na serikali na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu.
•    Awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya serikali ngazi ya mshahara TGS B.

NB: MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE

•    Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
•    Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, vyeti vya kidato cha nne au kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika pamoja na picha mbili (2) za passspoti.
•    Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25/11/2015.

Maombi yote yatumwe kupitia posta kwa anwani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P 52
MKUU-ROMBO


ENG, ANDREW TESHA
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO

1 comments: