Saturday, October 17, 2015
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/H/81 15 Oktoba, 2015
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa  Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 29 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

1.    AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (FOREIGN SERVICE OFFICER II) –NAFASI 8

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya kimahusiano ya kimataifa.
• Kuhudhuria mikutano mbalimbali.
• Kuandaa mahojiano.
• Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.
• Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
• Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao wamejiimarisha (major) katika fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations), Sheria au Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha wawe wamefanya na kufaulu mtihani unaotolewa Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D

2.    AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 3

MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
• Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
• Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa
na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi

3.    AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS OFFICER GRADE II) –NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Maafisa Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la :-
• Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na kusimamia matumizi ya kumbukumbu.
• Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala.
• Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, kutunza na kusimamia matumizi yake.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji na Uhifadhi wa Kumbukumbu (Records management & Archieves), Upimaji na Ramani na nyingine zinazolingana nayo kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.

4.    MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (NYARAKA) DARAJA LA II – (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI
• Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja I:-
• Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
• Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
• Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
• Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
• Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne (IV) au sita (VI) wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika fani ya Masjala.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi

5.    KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) – NAFASI 10

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.

6.    MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) – NAFASI 3

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuidhinisha hati za malipo.
• Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
• Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
• Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
• Kuandika taarifa ya maduhuli.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu (intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
AU
• Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

7.    AFISA HABARI II (INFORMATION OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI
• Kukusanya na kuandika habari.
• Kupiga picha.
• Kuandaa picha za maonyesho.
• Kuandaa majarida na mabango (Posters).
• Kukusanya takwimu mbalimbali.
• Kuandaa majarida na vipeperushi.
• Kuhifadhi picha na kuhudumia maktaba na marejeo.

SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu ya Uandishi wa Habari au sifa inayolingana nayo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

8.    MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
• Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
• Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
• Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
• Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi namaendeleo ya jamii.
• Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau

SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye shahada ya Uzamili ambao wamejiimarisha (major) katika
mojawapo ya fani ya Uchumi (Economics) au Fedha (Finance) kutoka Chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta

MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 30 Oktoba, 2015
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/  (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya
ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xv. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI WAKATI WA KUFANYA MAOMBI YA KAZI. ANUANI YA
BARUA HIYO ZIELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P
63100 DAR ES SALAAM