Saturday, October 03, 2015
MANISPAA YA ILALA

NAFASI ZA KAZI
Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Ilala anawatangazia wananchi/Wakazi wote wa Manispaa ya Ilala Nafasi Zifuatazo
1.Wasimamizi wa Uchaguzi wa Vituo
2.Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo
3.Makarani Waongozaji wa Kupiga Kura


Sifa za Muombaji
•    Awe Mtanzania
•    Awe Mkazi wa Kata atakayo fanyia Kazi
•    Kwa kazi ya Makarani waongozaji ikiwezekana awe wa kitu atakacho fanyia kazi
•    Awe na Umri wa Miaka 21 na Kuendelea
•    Awe na elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea

Jinsi ya kutuma maombi
NB: Barua zote zipelekwe kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata (AFISA Mtendaji wa Kata) wanazoombea kazi.

Isaya M.Mngurumi
Msimamizi wa Uchaguzi
Manispaa ya Ilala