Friday, October 02, 2015Position Description:
Mkurugenzi Mtendaji w Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anakaribisha maombi ya kazi kwa yeyote mwenye sifa katika kada zilizoainishwa hapa chini.

DEREVA III – TGOS A, NAFASI 7

SIFA

Awe raia wa Tanzania.
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne na mwenye leseni daraja “C” kutoka chuo cha ufundi VETA ama National Institute of Transport (NIT).
Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali.
Awe na cheti cha majaribio ya ufundi wa daraja la II na sifa zingine za ziada zinazohusiana na taaluma pamoja na kada hiyo.

Application Instructions:

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

Barua za maombi ziambatane na nakala za vyeti vya Elimu, Taaluma, Cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (passport).
Barua ziambatanishwe na maelezo binafsi ya mwombaji (CV)
Waombaji waliosoma nje ya nchi waambatanishe na uthibitisho wa vyeti kutoka baraza la mitihani ya taifa (NECTA).
Mwombaji awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Namba ya simu ya kiganjani na hasa kwa mitandao ya Vodacom na airtel.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14/10/2015.
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono.


Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W)

Godwin L. Benne
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
S.L.P 686
MLELE